Mapinduzi ya Teknolojia Kutoka Afrika: App ya Meseji inayoweza kuipiku Whatsapp

Huu ndio utandawazi katika karne ya 21 unavyoonekana: Mxit, kampuni ya Afrika, imetangaza dhamira yake ya kuingia katika soko la biashara nchini India, na kukabiliana ana kwa ana na ushindani kutoka kwa makampuni makubwa kutoka Marekani na yanayokuja kwa kasi kutoka China na Japan.
Mxit ndio watengenezaji wa app ya kutuma meseji (messaging app), ambayo kampuni hiyo inadai ina watumaiji takriban milioni saba unusu nchini Afrika Kusini, huku wengine wanaokaribia milioni 1 wakiwa nje ya nchi hiyo. Nchini India, Whatsapp inatumiwa na takriban watu milioni 35 ilhali app nyingine maarufu ya kutuma meseji, Line, ikitumiwa na watu tarkiban milioni 10. App nyingine maarufu ya WeChat kampuni ya Kichina nayo pia ina watumiaji wengi japo idadi yake kamili haijawekwa hadharani.
Sasa kipi kinaipa ‘kampuni ndogo’ kama Mxit ujasiri wa kudhani itamudu kuteka soko la apps za meseji nchini India? Jibu ni rahisi: visheni zaidi ya matumizi katika simu za kisasa (smartphones). Tofauti na ‘wapinzani’ wake ambao ni makampuni makubwa kama Whatsapp na Line, Mxit inaweza kutumika hata katika ‘simu za kawaida’ (yaani zisizo smartphone) ambazo ndizo zenye watumiaji wengi nchini India. Katika robo ya tatu ya mwaka jana, zaidi ya asilimia 80 zilizoingizwa India zilikuwa ‘za kawaida.’ Japo hali hii inabadilika- mwaka huu inatarajiwa mauzo ya simu za kisasa (smartphones) yatafikia simu milioni 225- lakini ‘simu za kawaida’ zinatarajiwa kuendelea kutawala soko.
Sababu kubwa ya umaarufu wa Mxiti nchini Afrika Kusini ni uwezo wake wa kutumika katika ‘simu za kwaida,’ huku hata simu zinazotumia mtandao ‘wa zamani’ wa 2G (mitandao maarufu kwa sas ani 3G na 4G) na ambazo hazikuundwa kwa ajili ya matumizi ya intaneti kwenye simu zikiweza kutumia app ya Mxit.Hii inasaidia kuwavuta watu wengi wenye marafiki wengi wanaotumia ‘simu za kawaida’ hupendelea kutumia huduma itakayowasaidia kuwaunganisha na marafiki zao wote, sio wale wenye simu za kisasa pekee.Katika nchi zisizo tajiri sana, kama Afrika Kusini na India,uwezekano wa watu kutumia simu za aina mbalimbali ni mkubwa zaidi kuliko katika nchi za Magharibi ambako soko la simu limeshajaa (saturated).
Kwa bahati nzuri, matumizi ya apps za kutuma meseji sio ‘mchezo wa jumla sifuri’ (kwa kimombo zero-sum game, yaani mazingira ambapo katika chochote kinachopatikana upande mmoja, kuna kinachopotea upande mwingine). Watu hupendelea kutumia apps mbalimbali za kutuma meseji katika kuwasiliana na marafiki wa aina mbalimbali pia. Lakini apps zinazofanikiwa ni zile zinazoelewa mahitaji ya watumaji wake. Na kampuni kama Mxit inayotoka dunia inayoendelea (developing world)- Afrika Kusini- inaweza kuelewa vyema mahitaji ya wateja katika nchi nyingine ya dunia inayoendelea- India. Imetafsiriwa kutoka QUARTZ

No comments:

Post a Comment

Pages